Salamu - Julai, 2026

Bwana Yesu Kristo asifiwe.. Tunamshukuru Mungu. Tumepewa mwezi huu wa saba kwa neema yake.
Katika mwezi uliopita tulikua na semina nyingi ..tulikua na semina Dodoma Mvumi na tukaenda Manyoni na Itigi huko Singida.. Asanteni kwa maombi na kwa sadaka zenu
Hivi ninapokutumia salamu tupo Ubaruku Mbalarini siku ya pili, tunasemina nzuri sana..Tuombeeni sana. Tukimaliza tutaenda Chimala ..Semina hizo ziko ndani ya mwezi huu wa saba.
Hebu tuanze kuzipokea salamu za mwezi huu wa sita.. Kumbuka tuna salamu zenye kichwa
JIFUNZE KUTAKA KARAMA AU KUOMBA MUNGU AKUPE KARAMA YA MIUJIZA NA UPONYAJI ( SEHEMU YA PILI)
5:MUNGU ANAWEZA TUMIA MUUJIZA ILI AMDHIBITISHE AU KUMTAMBULISHA MTUMISHI WAKE.
Ukisoma Biblia utajifunza kuwa Mungu ana tabia ya kuwa tambulisha watumishi wake. Ana njia nyingi za kuwatambulisha watumishi wake.
Moja ya mbinu anayoweza kuitumia ni Muujiza au ishara..Ni vema Mungu akutambulishe wewe kwa watu kuwa ni mtumishi wa Mungu, si vema wewe uwatambulishe watu kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu..
Mungu anapotaka kumtambulisha mtu anaweza kupitisha miujiza mikononi mwa huyo mtu..
Angalia mfano huu wa Bwana Yesu Kristo kama mtumishi wa Mungu.“22 Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;”( Mdo 2:22)
Kwa mujibu wa mistari hii utaona kuwa Mungu alimdhihirisha Bwana Yesu Kristo kuwa ni mtumishi wake kwa kutumia miujiza na ishara na ajabu.
Angalia na mistari hii mingine “4 Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.”( Waebrania 2:4)
Angalia hapo,utaona Mungu aliwashuhudia watu kwa kutumia miujiza ili kuwajulisha hao watu kuwa watumishi hao wapo pamoja na Mungu. Kwalugha nzuri alitumia miujiza ili kuwatambulisha watumishi wa Mungu
Angalia mfano huu mwingine,” 36 Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako.37 Unisikie, Ee BWANA, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, BWANA, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie.38 Ndipo moto wa BWANA ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji.”( 1Wafalme 18:36-38)
Nabii Eliya aliomba kwa Mungu amdhihilishe kama ni mtumishi wa Mungu.Angalia Mungu alitumia muujiza wa moto kushuka ili pia awajulishe wana wa Israeli kuwa Eliya ni mtumishi wa Mungu.
Kumbuka unaposoma Biblia utaona kipindi hicho kulikuwa na mashindano kati ya watumishi wa baali na Eliya.
Heshima ya Eliya kama mtumishi wa Mungu ilipotea, angalia watumishi wa baali walikuwa mia nne, yeye alikuwa peke yake.
Ukitazama idadi ya watumishi wa miungu walivyokuwa wengi unapata picha kuwa Waisraeli karibu wote walikuwa wengi sana.
Nabii Eliya alipoangalia jambo hilo alifikiri kuwa alikua peke yake, Mungu alimwambia kuna watu elfu saba walikuwa hawaabudu miungu.
Jambo hilo lilimfanya Eliya aombe kwa Mungu amtambulishe mbele ya wana wa Israeli kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu.
Sikia Mungu akigundua kuwa utumishi wa mtu wake hautambuliki mbele ya watu fahamu anaweza kumtambulisha huyo mtumishi kwa kutumia miujiza.
Sikia mtumishi,ikiwa watu wanakutambua wewe kuwa ni mtumishi wa Mungu haina haja ya kutafuta utambulisho kutoka kwa Mungu kwasababu hao watu wanakutambua wewe kuwa ni mtumishi wa Mungu.
Angalia na mistari hii “31 Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya BWANA juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha BWANA, wakamwamini BWANA, na Musa mtumishi wake.” (Kutoka14:31)
Ili watu wa mwamini mtumishi wa Mungu katika utumishi wake Mungu alitumia muujiza. Wana wa Israeli walipoiona kazi kubwa ya Mungu aliyoifanya mikononi mwa Musa wakaanza kumwamini.
Sikia unaweza ukawa wewe ni mtumishi wa Mungu yeye akakuamini lakini watu wasikuamini kabisa.
Mungu akiona hivyo anaweza kutumia mbinu kama hiyo ili watu hao waanze kumwamini mtumishi wa Mungu. Usisite kuomba Mungu akupe karama ya miujiza na uponyaji ili watu waanze kuwaamini watumishi wa Mungu.
Naamini umenielewa.. Tuonane katika salamu za mwezi ujao

Ukihitaji masomo yetu, unaweza kuyapata kwa njia zifuatazo:

1. App yetu ya huduma yenye jina “HUSONEMU (MWAKATWILA)” — inapatikana Play Store, ambapo kuna masomo mengi sana.

2. Tovuti yetu: www.mwakatwila.org

3. YouTube: HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU

4. Facebook: ingia kwenye tovuti yetu uone alama ya Facebook (f), kisha “like” ili upate maelezo ya kujiunga, au tafuta “SOMA NENO LA MUNGU”

5. Instagram: tafuta “Huduma ya Soma Neno la Mungu”

6. DVDs 📀 au CDs 💿

7. Vitabu

NB: Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733 ili kupata vitabu, DVD na CD.

8. Kwa njia ya redio:

  • Rungwe FM 102.5 MHz — Jumapili saa 3:00 hadi 4:00 usiku
  • Baraka FM 107.7 MHz — Jumanne saa 12:00 jioni hadi 1:00 usiku
  • Bomba FM 104.1 MHz — Ijumaa saa 3:00 hadi 4:00 usiku

9. Online Radio: radio.mwakatwila.org

Ratiba ya vipindi:

  • Saa 12:00 asubuhi
  • Saa 07:00 mchana
  • Saa 12:00 jioni
  • Saa 03:00 usiku

10. Ingia MWAKATWILA YouTube Online

Kwa mawasiliano zaidi:

+255 754 849 924
+255 756 715 222

Wako,
Mwl. Steven Mwakatwila & Beth Mwakatwila